Sheikh wa Mkoa wa Mkoa Mbeya, Msafiri Njalambaha amesema kitendo anachokifanya Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani na Spika wa Bunge Dkt. Tulia kuigusa jamii ni sadaka na kutekeleza maagizo ya Mungu visihusishwe na masuala ya kisiasa.
Sheikh Njalambaha amesema usiku wa jana Aprili 8 mwaka huu wakati wa waumini wa dini ya kiislam, viongozi wa Chama, Serikali na Machifu mkoani hapa walipoungana kula aftari iliyoandaliwa, Dkt. Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust.
Amesema Dkt. Tulia amekuwa msaada mkubwa kwa dini ya kiislam kwani licha ya kuwafutulisha pia amekuwa akichangia ujenzi wa misikiti, jamii yenye mahitaji.
“Tunaona mchango wake mkubwa, sio sasa ni zaidi ya miaka mitatu anatoa futari kwa waumini wenye hali duni na hivi karibuni tumepokea mchele kilo 400 tende katoni 20 hii ni sadaka isihusishwe na masuala ya kisiasa” amesema.
Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela amesema CCM imetulia na Dkt. Tulia na kwamba watamlinda na kuhakikisha uchaguzi Mkuu 2025 anapitia kwa kishindo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amemtaja Dkt. Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini kuwa ni kiongozi wa kuigwa na mfano amekuwa chachu ya kuleta maendeleo katika Jimbo la Mbeya na Mkoa kwa ujumla.
“Tunayaona anayofanya ameweza kujenga nyumba saba kwa wahitaji, kutoa sare za shule kwa watoto 3,000 kujenga misikiti na hata jitihada zake kuleta miradi mikubwa ikiwoeo barabaraa njia nne na stendi kubwa ya kisasa ya mabasi ya Mikoa, kama CCM tutamlindaa hao wengine waachane na siasa wakafanye biashara”.
Mwenyeki wa CCM, Mkoa Patrick Mwalunenge ameunga mkono kauli ya viongozi hao na kwamba watamlinda Dkt. Tulia Ackson kuendelea na majukumu ya Bunge wao wanachama kazi jimboni.
Recent Posts
- Online Casino Bonuses: Ho…September 25, 2026Online casino bonuses can add value to a gaming session, but the headline amount rarely tells the […]
- Online Casino Deutschland…September 25, 2026Online Casinos bieten heute eine große Auswahl an Spielautomaten, Tischspielen und […]
- Cazeus no deposit bonus c…September 25, 2026cazeus no deposit bonus codes – praktische gids voor Nederlandse spelers Ben je op zoek naar een […]
- Cazeus bonus registratie …September 25, 2026“`html Cazeus bonus registratie stappen – volledige gids voor Nederlandse spelers Cazeus […]
- Cazeus NL review: registr…September 25, 2026Cazeus NL – Alles wat je moet weten Na een pakkende hero‑afbeelding op de bovenkant van de pagina, […]






