SHEKHE NJALAMBAHA: DKT. TULIA NI ZAIDI YA MWANASIASA

Na Esther Macha, TimesmajiraOnline,Mbeya

SHEKHE wa Mkoa wa Mbeya,Msafiri Njalambaha amesema kitendo kinachofanywa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Spika wa Bunge ,Dkt.Tulia Ackson mbali na masuala ya kisiasa ni ibada kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwani amekuwa akijitolea kusaidia watu wenye uhitaji.

Shekhe Njalambaha amesema hayo leo,Aprili 4,2024 wakati akipokea kilo 400 za Mchele na Tende boksi 20 kutoka Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Mkurugenzi wake Dkt.Tulia ambapo makabidhiano hayo yamefanyika katika Msikiti wa mkoa uliopo eneo la Sokomatola Jijini hapa.

“Jambo hili ambalo linafanyika hapa la kupokea futari kwa niaba ya waislam wenye uhitaji kwa mkoa wa Mbeya toka kwa Dkt.Tulia kweli ni kitu ambacho kinaonyesha mtu anajitoa kwa ajili ya Mungu wake,tumsichukulie kiongozi kama mwanasiasa tu bali pia ni hisia na huruma ambayo kuna watu wenye uhitaji katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani jambo hili linatoa uhalisia wa Dkt.Tulia katika masuala ya kujisogeza kwa MUNGU wake ” amesema Shekhe Njalambaha.

Hata hivyo amesema kuwa watu wengine wanaweza kusema anafanya hayo kwa ajili ya siasa na kama ingekuwa nguvu ya soda mpaka Sasa ni zaidi miaka mitatu wamekuwa wamekuwa wakipokea shehena kubwa mpaka tani tano ambayo imekuwa mwendelezo kila mwaka na kwamba hilo jambo limejikita katika moyo wake kuona namna gani anaishi vipi na binadamu wenzie na watu anaowaongoza ili aweze kuwasaidia.

Aidha Shekhe Njalambaha amesema anamuombea Dkt.Tulia kwa kuweka utamaduni mzuri wa kujiweka karibu na Mwenyezi MUNGU ukiachana na siasa pia aliwaasa viongozi wengine kuiga mfano wa Dkt.Tulia .

Kwa upande wake Imamu wa Msikiti wa Baraa Bin Azb Isanga,Shekhe Ibrahim Bombo amesema kuwa katika kuelekea uchanguzi wa serikali za mitaa ni muhimu kuwepo na utulivu na amani na kwamba ni kipindi ambacho kitahitajika Dua kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Kipindi ambacho tunaelekea kwenye chaguzi za serikali za mitaa huwezi kujua watu watakuwa na mihemko kiasi gani lakini kwa kumuomba mwenyezi MUNGU kuleta utulivu na amani kwa kipindi hicho kikifika ni jambo la msingi ili kuendelea kunehemeka na keki ya Taifa”amesema Shekhe Bombo.

Aidha amesema kuwa kwa Dkt.Tulia imekuwa desturi yake kutoa sadaka kwa ajili ya wahitaji katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na desturi hiyo imekuwa endelevu .

Kwa upande wake Ofisa habari na mawasiliano na Taasisi ya Tulia Trust,Joshua Mwakanolo aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Rais umoja wa mabunge amesema wametoa msaada wa mchele kilo 400 na Tende boksi 20 ambazo alikabidhi kwa Shekhe mkuu ili aweze kuwapatia waumini wanaoishi katika mazingira magumu .

“Nimesimama kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini ,Spika wa Bunge ambaye pia ni Rais wa umoja wa Mabunge duniani Dkt.Tulia Ackson ili niweze kukabidhi futari hii kwa waumini “amesema.

Hata hivyo baada ya shekhe Nyalambaha kupokea msaada huo walifanya dua ya kumwombea Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson na Spika wa Bunge na Rais umoja wa mabunge duniani ili aweze kufanya kazi zake vizuri katika majukumu yake ya kila siku.

soma zaidi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

DONATE

Give us a call or fill in the form below and we'll contact you. We endeavor to answer all inquiries within 24 hours on business days. DONATE BY BANK: Account Name: TULIA TRUST Account Number: 0150226766000 Bank Name: CRDB