Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametoa ahadi ya kumpatia matibabu ya mguu Mzee mwenye mahitaji Mbaliki Shikunzi(80).
Shikunzi ambaye ni Mkazi wa mtaa Isengo Kata ya Iziwa Jijini hapa ambaye amekuwa na changamoto ya tatizo la kidonda mguu na kuishi katika mazingira magumu na kukosa msaada ikiwepo chakula, makazi hararishi.
Akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Ofisa Habari na Mawasiliano Joshua Mwakanolo amesema Dkt. Tulia amehaidi kumsaidia mhitaji huyo matibabu katika Hosptali ya Rufaa Kanda sambamba na kumjengea nyumba.
Mwakanolo ametoaa kauli hiyo jana Jumapili Aprili 7 mwaka huu wakati ajitosa msaada wa mahitaji ikiwepo mchele, unga,sukari na sababu.
“Tumekabidhi msaada wa chakula mchele kilo 20, unga wa ugali kilo 20, maharage kilo 10, sukari mifuko 3, sabuni miche 2, mafuta ya kupakaa sambamba na mavazi” amesema.
Shikungu anaishi kwenye mazingira magumu yanayopelekea kukosa mahitaji hayo muhimu na kuishi kwenye nyumba chakavu ambayo inaweza kuhatarisha maisha yake.
Mkurugenzi wake, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini DkT. Tulia Ackson imeahidi kumjengea nyumba ya kuishi pamoja na matibabu ya kidonda alichonacho mguuni katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.
Kwa upande wake mhitaji huyo ameshukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa mahitaji ikiwepo ahadi ya kumpatia matibabu na kumjengea makazi bora.
Recent Posts
- Lorem ipsum dolor sit ame…September 23, 2026Lorem ipsum dolor sit amet consectetur adipiscing elit. Quisque faucibus ex sapien vitae […]
- How Video-Led Casino Cont…September 23, 2026Choosing an online casino often starts with a practical question: what will the experience actually […]
- Casino BetOranje: stap‑vo…September 23, 2026BetOranje Casino – Praktische Gids voor Nederlandse Spelers 1. Over BetOranje: licentie, veiligheid […]
- BetOranje betrouwbaar: co…September 23, 2026BetOranje – Betoranje betrouwbaar: Alles wat je moet weten BetOranje: een korte introductie en […]
- BetOranje online casino a…September 23, 2026BetOranje online casino – Praktische gids voor Nederlandse spelers Registratie en eerste stappen […]






