TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

Taasisi ya Tulia Trust imetoa mifuko mia nne kwa shule tatu za msingi na sekondari Jijini Mbeya kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya madarasa katika shule hizo.

Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na Shule ya Msingi Mlimani iliyopo Kata ya Sinde,Sekondari ya wasichana ya Dkt Tulia ilioyopo Kata ya Iyunga na Sekondari ya Itende inayomilikiwa na Jumuia ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)iliyopo Kata ya Itende Jijini Mbeya.

Shule ya msingi ya Mlimani iliyopo Kata ya Sinde Jijini Mbeya imepokea msaada wa mifuko mia mbili kutoka Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Dkt Tulia Ackson Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.

Saruji hiyo imekabidhiwa na Afisa habari Joshua Mwakanolo kwa niaba ya Spika lengo ni kutekeleza ahadi zake baada ya kutembelea shule mbalimbali Jijini Mbeya

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Jane Mwaisumo anatoa shukurani zake mbele ya hadhara akisema Taasisi ya Tulia Trust imekuwa na msaada mkubwa kwenye jamii hususani shule ya Jijini Mbeya.

Diwani Kata ya Sinde Fanuel Kyanula amesema Dkt Tulia amekuwa akitoa misaada mbalimbali kwenye Kata yake yakiwemo madawati.

Akikabidhi saruji mifuko mia sekondari ya wasichana Dkt Tulia  Joshua Mwakanolo Afisa Habari wa Taasisi hiyo amesema lengo ni kutekeleza ahadi ya Mbunge baada ya kutembelea shule hiyo ambapo awali Dkt Tulia Ackson aliichangia shule hiyo shilingi milioni mbili kwa ajili ya ukarabati wa madarasa.

Mkuu wa shule hiyo Daud Mwaijibe ametoa neno la shukurani kwa Taasisi ya Tulia Trust akisema msaada huo utakuwa kichocheo cha elimu kwa shule hiyo.

Bertha Gerald kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji amesema Jiji linatambua mchango mkubwa unaotolewa na Dkt Tulia Ackson Jijini Mbeya.

Diwani wa Kata ya Iyunga Mwajuma Tindwa amesema Kata yake ilikuwa haina shule ya watoto wa kike hivyo maboresho yanayofanyika yataongeza ufaulu.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wamepata fursa ya kutoa neno la shukurani kwa Taasisi ya Tulia Trust wakisema msaada huo utawapunguzia michango.

Maboresho yanayofanyika katika shule hiyo hasa ujenzi wa mabweni umeinua ufaulu wa wanafunzi wa kike katika Kata ya Iyunga Jijini Mbeya ambapo matokeo ya kitaifa kidato cha pili na nne yamekuwa mazuri.

Katika hatua nyingine Taasisi ya Tulia Trust imetoa mifuko mia moja ya saruji kwa shule ya sekondari ya Wazazi Itende awali Mkuu wa shule hiyo Pyson Mwakalinga amesema msaada huo umekuja kwa wakati baada ya kuwasilisha maombi yao kwenye Taasisi hiyo.

Diwani wa Kata ya Itende Julius Malongo Mendagalile amesema Taasisi ya Tulia Trust isichoke kutoa misaada kwenye Kata yake.

Aidha Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Mbeya Jiji Emmanuel Mwalupindi amesema mara nyingi Dkt Tulia Ackson amekuwa kichocheo cha maendeleo kwenye Taasisi mbalimbali.

Nao baadhi ya wanafunzi wameshukuru kupata msaada huo na kuwa umetoa hamasa kwa wao kufaulu katika masomo.

Joshua Mwakanolo ni Afisa Habari wa Tulia Trust amesema Taasisi imejipanga kutekeleza maombi yote yaliyowasilishwa ofisini.

Shule ya Itende inakabiliwa na ukosefu wa maktaba kwa ajili ya wanafunzi kujisomea pamoja na maabara ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.

Fatu Chilundu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji amesema Dkt Tulia amekuwa msaada kwenye shule mbalimbali za Jiji la Mbeya.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sinde Silvester Mwanganya amesema Dkt Tulia anakiwakilisha vema Chama Cha Mapinduzi.

Diwani Kata ya Sinde Fanuel Kyanula amesema Dkt Tulia amekuwa akitoa misaada mbalimbali kwenye Kata yake yakiwemo madawati.

Baadhi ya wananchi wamempongeza Dkt Tulia kwa kutoa msaada wa saruji.

Shule ya Mlimani yenye watoto zaidi ya elfu moja licha ya upungufu wa madarasa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo kwa walimu na wanafunzi.

Akikabidhi saruji mifuko mia sekondari ya wasichana Dkt Tulia  Joshua Mwakanolo Afisa Habari wa Taasisi hiyo amesema lengo ni kutekeleza ahadi ya Mbunge baada ya kutembelea shule hiyo ambapo awali Dkt Tulia Ackson aliichangia shule hiyo shilingi milioni mbili kwa ajili ya ukarabati wa madarasa.

Mkuu wa shule hiyo Daud Mwaijibe ametoa neno la shukurani kwa Taasisi ya Tulia Trust akisema msaada huo utakuwa kichocheo cha elimu kwa shule hiyo.

Bertha Gerald kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji amesema Jiji linatambua mchango mkubwa unaotolewa na Dkt Tulia Ackson Jijini Mbeya.

Diwani wa Kata ya Iyunga Mwajuma Tindwa amesema Kata yake ilikuwa haina shule ya watoto wa kike hivyo maboresho yanayofanyika yataongeza ufaulu.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wamepata fursa ya kutoa neno la shukurani kwa Taasisi ya Tulia Trust wakisema msaada huo utawapunguzia michango.

Maboresho yanayofanyika katika shule hiyo hasa ujenzi wa mabweni umeinua ufaulu wa wanafunzi wa kike katika Kata ya Iyunga Jijini Mbeya ambapo matokeo ya kitaifa kidato cha pili na nne yamekuwa mazuri.

Katika hatua nyingine Taasisi ya Tulia Trust imetoa mifuko mia moja ya saruji kwa shule ya sekondari ya Wazazi Itende awali Mkuu wa shule hiyo Pyson Mwakalinga amesema msaada huo umekuja kwa wakati baada ya kuwasilisha maombi yao kwenye Taasisi hiyo.

Naye Meneja wa shule hiyo Abdul Sikitiko Komba ambaye ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi amesema msaada huo umewafuta machozi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya shule Kaseka William Wambali amesema msada uwe kichocheo cha ufaulu kwa wanafunzi.

Diwani wa Kata ya Itende Julius Malongo Mendagalile amesema Taasisi ya Tulia Trust isichoke kutoa misaada kwenye Kata yake.

Aidha Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Mbeya Jiji Emmanuel Mwalupindi amesema mara nyingi Dkt Tulia Ackson amekuwa kichocheo cha maendeleo kwenye Taasisi mbalimbali.

Nao baadhi ya wanafunzi wameshukuru kupata msaada huo na kuwa umetoa hamasa kwa wao kufaulu katika masomo.

Joshua Mwakanolo ni Afisa Habari wa Tulia Trust amesema Taasisi imejipanga kutekeleza maombi yote yaliyowasilishwa ofisini.

Shule ya Itende inakabiliwa na ukosefu wa maktaba kwa ajili ya wanafunzi kujisomea pamoja na maabara ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.

soma zaidi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

DONATE

Give us a call or fill in the form below and we'll contact you. We endeavor to answer all inquiries within 24 hours on business days. DONATE BY BANK: Account Name: TULIA TRUST Account Number: 0150226766000 Bank Name: CRDB