Taasisi ya Tulia Trust imeanza programu maalum ugawaji wa baiskeli za viti mwendo kwa walemavu sambamba na kuwaingiza kwenye mpango wa kuwezesha kiuchumi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubaini kundi kubwa la walemavu kuishi maisha ya tabu kwa kukosa usaidizi ikiwepo miradi ya kujipatia kipato cha kujikimu.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema leo Jumanne Machi 12, 2024 wakati akikabidhi kitimwendo kwa mlemavu Zaina Mbwalo (50) mkazi wa mtaa wa Kabwina Kata ya Sinde jijini hapa.
“Kupitia Mlemavu Zainabu tumebaini kuna mahitaji makubwa watakatiwa mitaji ili kuanzisha miradi ya kiuchumi”.
Mwakanolo amesema kama Taasisi waliweka malengo yao ni kutoa viti mwendo kwa walemavu kata 36 lakini baada ya kuanza zoezi imebainika wahitaji ni wengi.
Pia Taasisi hiyo imeweza kutoka madaftari katika Shule za Hasanga na Kilimo Bonge la Uyole ambapo pia imeelezwa mahitaji bado ni makubwa huku malengo yalikuwa kutoka kwa watoto 3,000 wenye mahitaji kutoka kaya zisizojiwe.
“Mahitaji ya Walengwa yamekuwa makubwa tofauti na tulivyitarajia lakini tutawafikia wahitaji wote wakiwepo walemavu na watoto wenye mazingira magumu mashuleni” amesema.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kiti mwendo, Mlemavu Zaina amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 30 ameishi kwa tabu licha ya kujihusisha na biashara ndogo ndogo.
“Nikitaka kutoka kufuata mahitaji nalazimika kuita vijana wanibebe na kulipa gharama kulingana na umbali huku akitoa mfano, kwenda kanisani ni Sh 4,000” amesema.
Amesema anamshukuru kwa msaada huo huku akieleza kuhitaji kiasi cha Sh 1 milioni ili kuagiza udongo wa kutengenezea majiko” amesema.
Recent Posts
- WANAFUNZI WAMTAJA DKT. TU…August 21, 2024Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]
- WALIOHITIMU ELIMU YA KIDA…August 21, 2024Wanafunzi watano waliokuwa wakisoma nchini Nigeria kwa ufadhiri wa Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wa Spika wa Bunge Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wamewasili leo Ijumaa Agost 16 mwaka huu.[…]
- 1,000 KUSHIRIKI MASHINDAN…August 21, 2024Mashindano hayo yanajulikana kama Tulia Cooking Festival yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi Agosti 2024 na yakishirikisha washiriki 1,000[…]
- WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO…May 22, 2024Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 11, 2024 ameshiriki katika tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathoni 2024[…]
- DKT. TULIA ATOA MSAADA KW…April 22, 2024Dkt.Tulia Ackson amekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa waathirika ambao nyumba zao zilifunikwa na maporomoko ya tope katika Mlimani Kawetele Kata ya Itezi jijini hapa na kusababisha kukosa makazi ya kuishi.[…]