TAASISI YA TULIA TRUST YAMKABIDHI KITIMWENDO MLEMAVU ALIBEBWA MGONGONI MIAKA SABA

Taasisi ya Tulia Trust leo imefanya matukio mawili likiwepo la kukabidhiwa madaftari  kwa watoto wenye mahitaji maalum 3,000 katika shule la za msingi kata 36 jijini hapa.

Akikabidhi msaada wa kitimwindo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema kuwa bado wataendelea kutoa viti mwendo kwa walemavu wenye uhitaji katika kata zote 36 za Jiji la Mbeya.

“Leo tumekuja kutoa misaada ya madaftari kwa wanafunzi 3,000 ambao walipata ya sare za shule za msingi kupitia Mkurugenzi wa Taasisi na  Spika wa Bunge, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya mjini ,Dk Tulia Ackson

Mwakanolo amesema kama Taasisi bado wataendelea kushirikiana na familia ya Doreen kuhakikisha anapata msaada mbalimbali sambamba na mzazi wake kuingizwa kwenye mpango wa kuwezesha  wajasirimali ili atunishe miradi wake na kuweza kumhudumia.

Akizungumza mara baada ya kupata msaada wa kitimwindo, Doreen ambaye alishindwa kujizuia na kububujikwa. machozi  amesema anamshukuru kwa msaada huo.

“Nilikuwa nikichelewa kufika shuleni wakati mwingine nikifika nakuta wenzangu wameanza masomo naomba serikali inisaidie nikimaliza elimu ya msingi nipete shule maalum” amesema.

Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo Ezekiel amesema kwa mwaka huu anatarajia kuhitimu elimu ya msingi wanaomba serikali kumtengenezea mazingira mazuri katika kuelekeza elimu ya Sekondari.

“Ni Mwanafunzi anayefanya vizuri kwenye masomo hivyo ili kutimiza malengo yake atengenezewe mazingira mazuri katika elimu ya Sekondari ikiwepo shule maalum za walemavu na sio za kata” amesema.

soma zaidi

 

Mbali na msaada huo pia imemgusa Mwanafunzi mlemavu wa miguu Doreen Myuki (12) anayesoma darasa la saba katika shule ya Msingi Mwasote Jijini hapa aliyekuwa akibebwa kwa miaka saba mgongoni akipelekwa shule na kurudi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

DONATE

Give us a call or fill in the form below and we'll contact you. We endeavor to answer all inquiries within 24 hours on business days. DONATE BY BANK: Account Name: TULIA TRUST Account Number: 0150226766000 Bank Name: CRDB