Taasisi inawakaribisha Watanzania wote kwenye mashindano ya riadha yajulikanayo kama MBEYA TULIA MARATHON msimu wa Nane mashindano yatafanyika mnamo tarehe 10-11/05/2024 uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kuanzia saa 12:00 asubuhi.
Ijumaa ya tarehe 10/05/2024 yatafanyika mashindano ya mbio fupi yaani M100, M200, M400, M800 na 1500M, ambapo siku ya Jumamosi tarehe 11/05/2024 yatafanyika mashindano ya mbio ndefu yaani KM5, KM10, KM21 na KM42 ikiwa ni pamoja na kukabidhi zawadi kwa washindi wote wa riadha kwa siku zote mbili.Pamoja na hayo tutakua na vituo kadhaa vya kuuzia namba za usajili ili uweze kushiriki kikamilifu kuwania ushindi wa MBEYA TULIA MARATHON 2024, Vifuatavyo ni vituo utakavyoweza kujisajili kushiriki Mbeya Tulia Marathon;
MKOA WA MBEYA.
- Tukuyu – Ofisi ya Tulia Trust +255 753 176328
- Uyole – Ofisi ya Tulia trust +255 755 682187
- Kyela – Ofisi ya Tulia Trust +255 769 737637
- Kabwe – Friendship Stationery +255 769 846832
- Mwanjelwa – Nasra House of Fashion +255 767 454772
- Mwanjelwa – Light Shop +255 769 300702
MKOA WA ARUSHA
Sheikh Amri Abeid Stadium +255 769 846832
Tunawakaribisha Wajasiriamali wote kutumia fursa hiyo ya kufanya biashara zao bila gharama yeyote, pamoja na hayo kutakua na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya pamoja na burudani za ki asili (ngoma za jadi), Maelezo zaidi piga simu namba +255 763 828271.
JOSHUA EDWARD
AFISA HABARI NA MAWASILIANO TULIA TRUST
Recent Posts
- Vegas Hero Casino: Zijn d…March 11, 2026Vegas Hero Casino, een dynamische speler in de online gokindustrie, heeft de aandacht getrokken van […]
- True Luck Casino offre-t-…March 7, 2026En tant qu’analyste en ligne spécialisé dans les casinos depuis plusieurs années, j’ai examiné avec […]
- Der Froggybet Kosmos: Ein…March 6, 2026Als SEO-Kopiräfter mit zehn Jahren Erfahrung im iGaming-Bereich habe ich viele Online-Casinos […]
- Lizaro Casino: een diepga…March 6, 2026Het lizaro online casino heeft zichzelf gepositioneerd als een aantrekkelijke optie voor online […]
- De gebruikersinterface va…March 6, 2026Million Casino is een interessante nieuwkomer in de online gokwereld, die zich richt op zowel […]






