Muktasari:
Kauli hiyo imetolewa na Shekhe wa Mkoa wa Mbeya , Shekhe Msafiri Njalambaha leo Jumatano Machi 19, 2025 baada ya kupokea futari kwa wahitaji 200 wa dini ya Kiislamu iliyotolewa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
Mbeya. Viongozi wa dini ya Kiislamu Mkoa wa Mbeya wamefanya dua maalumu ya kuliombea Taifa na viongozi wa Serikali akiwepo Rais Samia Suluhu Hassan katika kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
Mbali na dua hilo wakikemea baadhi ya Watanzania kujiepusha na fikra mbaya za kujihusisha uvunjifu wa amani
na badala yake kuombea utulivu na amani kwa maslai ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha ametoa kauli hiyo leo Jumatano Machi 19, 2025 baada ya kufanya dua maalumu na kupokea futari za wahitaji 200 iliyotolewa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kupitia Taasisi ya Tulia Trust.
Njalambaha amesema huu ni mwaka wa uchaguzi kama viongozi wa dini wanalojukumu kubwa kuungana na waumini
na Watanzania kuombea amani, utulivu na kukemea vitendo “Taifa letu limepata tunu ya viongozi wa ngazi za juu
wanawake akiwepo Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya, Dk Tulia Ackson, hivyo niwaombe Watanzania tuzitunze hizi tunu na tusikubali kuzipoteza,” amesema.
Wakati huo huo,Shekhe Njalambaha amewataka wananchi kutohusisha misaada inayotolewa na Mbunge wa Mbeya
mjini, Dk Tulia Ackson na masuala ya kisiasa kutokana na kuelekea kipindi cha uchaguzi. “Hii siyo mara ya kwanza kiongozi huyo kugusa wahitaji kila mwaka anatoa mahitaji katika kipindi cha mfungo wa Idd El-Fitr, niombe tu waumini na Watanzania kuendelea kumuombea na kuliombea Taifa akiwamo Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema.
Amesema matendo yanayofanywa, Dk Tulia kuigusa jamii ya Kimungu na siyo mara ya kwanza kugusa wahitaji.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza la Masheikhe Mkoa, Sheikh Ibrahim Bombo ameishukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa utaratibu wake wa kugusa walengwa huku akiwataka maimamu wa misikiti iliyoguswa kuhakikisha walengwa wanafikiwa. “Tuna kila sababu ya kushukuru kwa mahitaji ya walengwa 200 katika misikiti mbalimbali katika Jiji la Mbeya, jukumu letu ni kuendelea kufanya dua kumuombea,” amesema.
Mwakilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Athuman Kapuya ameshukuru ushirikiano wa viongozi wa dini na kuomba kuendelea kumuombea Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson.
Amesema wataendeleza ushirikiano unaogusa jamii yenye mahitaji katika mfungo na kuelekea Sikukuu ya Idd.
Mnufaika Stumahi Michuzi amesema wataendelea kufanya dua kumuombe Mbunge wa Mbeya, Dk Tulia, Mungu aendelee kumzidishia kutokana na namna anavyojitoa kugusa jamii yenye uhitaji.
Recent Posts
- Vegas Hero Casino: Zijn d…March 11, 2026Vegas Hero Casino, een dynamische speler in de online gokindustrie, heeft de aandacht getrokken van […]
- True Luck Casino offre-t-…March 7, 2026En tant qu’analyste en ligne spécialisé dans les casinos depuis plusieurs années, j’ai examiné avec […]
- Der Froggybet Kosmos: Ein…March 6, 2026Als SEO-Kopiräfter mit zehn Jahren Erfahrung im iGaming-Bereich habe ich viele Online-Casinos […]
- Lizaro Casino: een diepga…March 6, 2026Het lizaro online casino heeft zichzelf gepositioneerd als een aantrekkelijke optie voor online […]
- De gebruikersinterface va…March 6, 2026Million Casino is een interessante nieuwkomer in de online gokwereld, die zich richt op zowel […]






