
“Miaka ya nyuma wagonjwa waliokuwa wakipewa rufaa walikuwa wakisafirishwa lakini sasa huduma zote zinapatikana katika hosptali yetu ya Kanda na bado tunaendelea kupokea fedha kwa ajili ya kuendeleza huduma ikiwepo za wagonjwa wa dharura sambamba na vituo vya afya na zahanati” amesema.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, ameagiza Wizara ya afya, Hosptali, vituo vya afya na zahanati kuboresha na kuyasimamia madirisha ya wazee nchini.
Amewataka watoa huduma wasiwavunje Moyo wazee wanapofika kupatiwa huduma kwa kutambua kuwa ndio wamelifikisha taifa hapa lililo kwa ushirikiano na mshikamano.
Katika hatua nyingine amesema kama wabunge kitendo alichokifanya Dkt. Tulia kimewapa darasa kwa kutoa bima za afya kwa kaya 1,000 zenye watu 6,000.
Naye, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amechangia Sh 10 milioni kwa ajili ya kuendeleza mpango wa utoaji za bima za afya kwa wananchi wa jimbo la Mbeya kupitia Taasisi ya Mbunge wa Mbeya mjini, Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Amesema kitendo anachofanya Dkt. Tulia anawapa somo kwani amekuwa ni Mbunge anayejua anafanya nini licha ya kuwa kiongozi mkubwa kwenye dunia lakini kila akija ziara Mkoa wa Mbeya lazima anamkuta na anaeleza matatizo ya wananchi wake.
Kwa upande wake Mratibu wa zoezi la ugawaji wa bima za afya, Frank Kalinga amesema kwa kipindi cha miaka mitano wametoa bima za afya kwa kaya 2,670 zenye wahitaji 16,020 katika Mkoa wa Mbeya.
Amesema bado mahitaji ni makubwa na kumuomba Mkurugenzi wa Taasisi hiyo kuona namna katika awamu nyingine kuzifikia kaya nyingine zenye uhitaji.
Mnufaika wa mpango huo, Fredy Pondo ameshukuru Taasisi ya Tulia Trust kwani imeweza kuthamini maisha ya wananchi wa kipato cha chini kuwapatia bima za afya zitakazo wasaidia kupata huduma za afya bure.
Recent Posts
DKT. TULIA AHAMASISHA MAM…
May 30, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]DKT.TULIA AMEREJESHA FURA…
May 30, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]BENJA FC WABABE WA TULIA …
May 30, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]DKT. TULIA ASISITIZA MATU…
May 30, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]WANAFUNZI WAMTAJA DKT. TU…
August 21, 2024Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]