Wazee wasiojiweza Jijini Mbeya wameanza kutabasamu baada ya Taasisi ya Tulia Trust kuanza program ya kugawa chakula na mavazi bure.
Programu hiyo imeanza leo katika baadhi ya Kata lengo ni kuhakikisha wahitaji wanafikiwa huku kikosi kazi cha Taasisi ya Tulia Trust kikiendesha zoezi hilo kulingana na idadi ya waliobainika.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi hiyo, Joshua Mwakanolo amesema lengo ni kuhakikisha wazee wasiojiweza wanatabasamu kwa kupata mahitaji muhimu.
“Mpango huu ni kutekeleza maono ya Mkurugenzi wetu ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge, na Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Dkt. Tulia Ackson” amesema.
Amesema bado wanaenda kuhakikisha jamii inatabasamu ikiwepo ujenzi wa makazi bora kutoa viti mwendo kwa watu wenye walemavu.
Mkazi wa Jijini Mbeya, Lazaro Juma ameishukuru Taasisi hiyo akiwepo Mkurugenzi wake Dkt. Tulia Ackson kwa kugusa wazee waliosahaulika katika jamii na kuonekana ni wasumbufu.
“Ni mtu wa kipekee sana kwa kipindi kifupi amegusa jamii ya wenye mahitaji wakiwepo watoto wenye mazingira magumu kupata sare za shule, madaftari na hata ujenzi wa makazi bora kwa wahitaji jambo ambalo lina thawabu kubwa mbele za Mungu” amesema.
Recent Posts
- Online Casino Deutschland…September 24, 2026Mehr als die Höhe eines Bonus entscheidet darüber, ob ein Online Casino für deutsche Spieler […]
- Vbet Casino im analytisch…September 24, 2026Mehr als die Hälfte der Online-Casino-Spieler bewertet heute nicht mehr nur die Auswahl, sondern […]
- Online-Casinos in Deutsch…September 24, 2026Mehr als die Spielauswahl entscheidet über die Qualität eines Online-Casinos: Lizenz, […]
- Online-Casino im Check: S…September 24, 2026Ein Online-Casino wirkt auf den ersten Blick wie eine Spielhalle ohne Anfahrt, ohne Neonröhren und […]
- Online-Casino-Vergleich: …September 24, 2026Ein Online-Casino wirkt auf den ersten Blick wie ein blinkender Jahrmarkt: viele Symbole, schnelle […]






