TULIA TRUST YAGUSA WALEMAVU, WAZEE MAHITAJI YA CHAKULA NA KUBORESHA MAKAZI.

Taasisi ya Tulia Trust imekabidhi mahitaji ya chakula kwa wahitaji Wilayani Rungwe  kwaajili ya Sikukuu ya Krismasi. Msaada huo uliokabidhiwa kwa kaya 13 ni pamoja na mchele, maharage na mafuta ya kula vyenye jumla ya thamani ya Sh. milioni 3.

Ofisa habari na Mawasiliano wa taasisi hiyo Joshua Mwakanolo amesema walengwa walionufaika ni ambao walibainika kwenye siku saba za kukimbiza bendera ya Upendo, Uwajibikaji na Mshikamano.

“Wahitaji hao walibainika kupitia mbio za bendera hiyo kutoka Tulia Trust zilizofanyika wilayani Rungwe zilizobeba Ujumbe wa kuhamasisha Upendo, Uwajibikaji na Mshikamano” amesema Mwakanolo.

Amesema mpango huo wa taasisi umetolewa  kupitia program ya Tulia Trust Mtaani Kwetu ambayo inalenga kuwasaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Mwakanolo amesema mbali na misaada huo wa chakula pia wameanza ujenzi na ukarabati wa makazi ya walemavu na wazee wanaoishi kwenye makazi hatarishi.

“Kuna nyumba za mahitaji wiwili tumeanza ujenzi baada ya kubaini makazi yao sio salama na kuwa katika hatari na haya ni maelekezo ya Mkurugenzi wa taasisi Dkt. Tulia Ackson na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika kuisaidia jamii” amesema Mwakanolo.

Mwakanolo amesema lengo la taasisi hiyo ni kuona jamii hususani wazee na walemavu wanakuwa sehemu salama kama jamii nyingine ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali kuondoa changamoto kwa watanzania wenye mahitaji.

Kwa upande wake kikongwe Never Kisuru (80) amemshukuru Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa moyo wa kujitolea kwa wenye mahitaji pasipo kujali itikadi vya vyama wala udini.

“Maisha yangu nilikuwa naishi kwenye nyumba ya mianzi lakini leo hii taasisi hii baada ya kunitembelea nimeanza kujengwa makazi bora ambayo  yataniwezesha kuwa salama” amesema Kisuru.

https://mbeyapresstv.blogspot.com/2023/12/tulia-trust-yagusa-walemavu-wazee.html

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

DONATE

Give us a call or fill in the form below and we'll contact you. We endeavor to answer all inquiries within 24 hours on business days. DONATE BY BANK: Account Name: TULIA TRUST Account Number: 0150226766000 Bank Name: CRDB