Tulia Trust > News > Community Assistance > TULIA TRUST YAKABIDHI KITI MWENDO KWA MLEMAVU ALIYESOTA MIAKA SABA RUNGWE.
TULIA TRUST YAKABIDHI KITI MWENDO KWA MLEMAVU ALIYESOTA MIAKA SABA RUNGWE.
Taasisi ya Tulia Trust imekabidhi kiti mwendo kwa mtoto Ester Seme (7) mkazi wa kijiji cha Ilolo Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya alipata ulemavu tangu akiwa na umri wa mwaka mmoja mara baada ya kumpoteza mama yake mzazi.
Kiti hicho kimekabidhiwa jana na Ofisa Uhusiano na Mawasiliano, Joshua Mwakanolo kwa bibi wa mlemavu huyo Justina Seme (80) kwa lengo la kumsaidia kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Pia Mwakanolo alikabidhi bendera yenye ujumbe maalum wa uwajibikaji, upendo na ushirikishwaji kwa jamii ikiwa ni maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi kitimwendo, Mwakanolo amesema kitendo hicho ni kuikumbusha jamii kurejea kwenye dhana ya uwajibikaji, upendo, mshikamano na ushirikiano. Mwakanolo amesema umefika wakati sasa watanzania kuenzi utamaduni wetu kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya katika kusukuma mbele maendeleo ya watanzania. “Tutakuwepo kwa kipindi cha siku saba (wiki moja) kupeperusha bendera sambamba na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii na elimu ya dhana nzima ya Uhuru wa Tanganyika” amesema.Akizungumza mara baada ya kupokea kitimwendo, Jestina Seme amesema analia machozi ya uzuni na furaha kwani hakikutarajia ipo siku mjukuu wake atakumbukwa na kupata matumaini ya kutoka nje na kujumuika na jamii nyingine” amesema. Amesema kuwa mama mzazi wa Ester alifariki mwaka 2016 alimuacha akiwa na mwaka mmoja na kuendelea kulea katika mazingira magumu kwani baba yake mzazi ajulikani alipo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Ilolo, Seti Bukuku amesema Dkt. Tulia Ackson amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Rungwe licha ya kuwa Mbunge wa Mbeya mjini, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Tanzania. “Wanarungwe tunaendelea kumuombea kwani ametugusa sana kwa msaada wa utoaji wa viti mwendo sana kwa mtoto, Ester familia yake ilikuwa katika kipindi kigumu cha kumsaidia miaka saba akiwa mlemavu” amesema.
https://mbeyapresstv.blogspot.com/2023/12/tulia-trust-yakabidhi-kiti-mwendo-kwa.html
Recent Posts
- WANAFUNZI WAMTAJA DKT. TU…August 21, 2024Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]
- WALIOHITIMU ELIMU YA KIDA…August 21, 2024Wanafunzi watano waliokuwa wakisoma nchini Nigeria kwa ufadhiri wa Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wa Spika wa Bunge Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wamewasili leo Ijumaa Agost 16 mwaka huu.[…]
- 1,000 KUSHIRIKI MASHINDAN…August 21, 2024Mashindano hayo yanajulikana kama Tulia Cooking Festival yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi Agosti 2024 na yakishirikisha washiriki 1,000[…]
- WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO…May 22, 2024Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 11, 2024 ameshiriki katika tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathoni 2024[…]
- DKT. TULIA ATOA MSAADA KW…April 22, 2024Dkt.Tulia Ackson amekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa waathirika ambao nyumba zao zilifunikwa na maporomoko ya tope katika Mlimani Kawetele Kata ya Itezi jijini hapa na kusababisha kukosa makazi ya kuishi.[…]