MASHINDANO YA MBEYA TULIA MARATHON KUTIMUA VUMBI MEI 10 NA 11 SOKOINE, JIJINI MBEYA

Mratibu wa Mashindano ya Mbeya Tulia Marathon, Lwiza John akionyesha sehemu ya  medali zitakazolewa kwa washindi wa mbio hizo zitakazofanyika Mei 10 na 11 mwaka huu.

Mashindano ya mbio za riadha maarufu kama  Mbeya Tulia Marathon yanatarajia kuanza kutimua vumbi katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya Mei 10 mpaka 11 mwaka huu.
Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust ambayo Mkurugenzi wake ni Rais wa Mabunge Duniani (IPU) ambae pia ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi hiyo, Joshua Mwakanolo amesema mashindano hayo yatahusisha mbio fupi na ndefu.
Amesema Mei 10 mwaka huu yatafanyika mashindano ya mbio fupi za mita 100, mita 200, mita 400 mita 800 mpaka mita 1500.
Mwakanolo amesema Mei 11 mwaka huu yatafanyika mashindano ya mbio ndefu za kilometa tano 43 ikiwa ni pamoja na kukabidhi zawadi kwa washindi wote wa walioshiriki  kwa siku zote mbili.
“Mbali na maandalizi ya mbio hizo kutakuwepo na vituo vya kuuzia namba za  usajili wa kushiriki ili waweze kushiriki kikamilifu kuwania ushindi wa Mbeya Tulia Marathon 2024 ” amesema Mwakanolo.
Wakati huo huo ametaja vituo ambavyo vitakuwa na namba za usajili kuwa ni Tukuyu Wilaya ya Rungwe, Uyole, Kyela katika Ofisi za Tulia Trust, na Kabwe Mwanjelwa.
Amesema kwa upande wa mbio ndefu mshindi wa kwanza atapata Sh milioni mbili, mshindi wa pili milioni moja, na mshindi wa tatu atapata  laki saba, mshindi wa nne atapata laki nne na mshindi wa tano atapata laki mbili huku wengine watano wakipata kitita cha Sh laki moja.
Ametaja washindi wa mbio fupi mshindi wa kwanza atapata Sh milioni 1.3, mshindi wa pili atapata laki tano, mshindi wa tatu atapata laki tatu, mshindi wa nne atapata laki moja na elfu arobaini, mshindi wa tano atapata laki moja.
Kwa upande wake Mratibu wa mashindano hayo, Lwiza John amesema msimu huu ni wa kitofauti kwani wanatarajia kupokea washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini.
“Mbali na kitoa kitita cha pesa pia kuna Medali zitatolewa pia anawakaribisha wananchi wa Mbeya kushiriki mashindano hayo kwani ni fursa pekee ambayo itaibua washindi ambao watatoka na vibunda” amesema Lwiza.
Naye Ofisa michezo na utamaduni Jiji la Mbeya, Joyce Mwakifwamba amesema  Mbeya Tulia Marathon kwa msimu huu imekuja kitofauti na kumtaka washiriki kujitokeza kwa wingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

DONATE

Give us a call or fill in the form below and we'll contact you. We endeavor to answer all inquiries within 24 hours on business days. DONATE BY BANK: Account Name: TULIA TRUST Account Number: 0150226766000 Bank Name: CRDB