Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson amekemea tabia ya baadhi ya familia kuwa na utamaduni wa kutelekeza wazazi kwa kutanguliza imani za kishirikina.
Dkt. Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mbunge Duniani (IPU) amesema jana Novemba 11, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa mtaa wa Inyara Kata ya Iyunga.
Kauli ameitoa wakati akikabidhi nyumba kwa wajane Tusekile Lumbalile (88) na Mwaine Lumbalile (86) ambao ni ndugu wa familia moja wanaoishi bila msaada wa familia.
“Ndugu zangu inaumiza sana hawa wakina mama walipaswa watunzwe na familia zao lakini wanaishi peke yao huku changamoto ni kujengeka na kuamini imani potofu za kishirikina” amesema.
Ameongeza “Namuomba Mungu hao watoto walio zaliwa na wazee, awatunze wapate familia ambazo wakifika nao uzeeni wawafanye kama wanavyo watenda wazazi wao” amesema.
Dkt. Tulia ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kisaidia wazee wasio jiweza na sio kuwaacha wakipitia maisha magumu kutokana na dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa wananchi na familia zao.
Mbunge wa Jimbo la Mbarali Bahati Ndingo amewataka wanambeya kuitumia tunu ya Dkt. Tulia kama mwanga katika kuisaidia jamii na kuleta maendeleo kwa wananchi.
“Mimi jimboni kwangu nahojiwa lini nitasaidia wananchi kama anavyofanya, Mbunge wenu niwasihi tu shikamane na kumuunga mkono” amesema Ndingo.
Recent Posts
- Online Casino Deutschland…September 25, 2026Online Casinos bieten heute eine große Auswahl an Spielautomaten, Tischspielen und […]
- Cazeus no deposit bonus c…September 25, 2026cazeus no deposit bonus codes – praktische gids voor Nederlandse spelers Ben je op zoek naar een […]
- Cazeus bonus registratie …September 25, 2026“`html Cazeus bonus registratie stappen – volledige gids voor Nederlandse spelers Cazeus […]
- Cazeus NL review: registr…September 25, 2026Cazeus NL – Alles wat je moet weten Na een pakkende hero‑afbeelding op de bovenkant van de pagina, […]
- Cazeus in Nederland – vol…September 25, 2026Cazeus – Praktische gids voor Nederlandse spelers Op zoek naar een betrouwbaar online casino dat […]






