Mjane Sigwava Jackson (60) amemshukuru Mbunge wa Mbeya mjini, Spika wa Bunge na Rais wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia kwa kumtupia jicho na kumjengea makazi bora.
Sigwava Mkazi wa mtaa Itanji Kata ya Iganjo Jijini Mbeya amepata tabasamu hilo baada ya Taasisi ya Tulia kupitia mpango wa Tulia Trust mtaani kuboa makazi ya awali ambayo yalikuwa hatarishi na kumjengea nyumba ya kisasa.
Hata hivi ameshindwa kujizuia hisia zake kwa kumshukuru Dkt. Tulia kuwa hatua hiyo ya kuwatoa kwenye mazingira hatarishi waliyopitia .
Akizungumza ujenzi wa nyumba Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo amesema ujenzi huo umeanza jana Machi 20 mwaka huu na utakamilika mwezi wa nne mwaka huu.
“Tunatarajia ndani ya mwezi mmoja itakuwa imekamilika na Mkurugenzi wa Taasisi ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson” amesema Mwakanolo.
Mwakanolo amesema program wamewafikia wahitaji zaidi ya sita kwa Mkoa wa Mbeya na ni zoezi endelevu makundi hayo wakiwepo wazee, wajane, wagani, walemavu na yatima.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Itanji Kata ya Iganjo amesema amemtaja, Dkt. Tulia kuwa mfano wa kuigwa na manufaa kwa wananchi wa Jimbo la Mbeya kwa kugusa jamii yenye uhitaji.
Mtendaji wa Mtaa Itanji Lucy Mwinuka ametoa wana kila sababu ya kuendelea kumuombea kwani amekuwa ni Mbunge wa kipelee kucha ya kuwa na nafasi kubwa duniani lakini amekuwa anajishusha sana kwa wananchi wa chini.
Diwani wa Kata ya Iganjo Eliud Mbogela amepongeza juhudi za Dkt. Tulia Ackson kwa wananchi wake na kutaka viongozi wengine kuigwa mfano huo ambao imekuwa na thawabu kubwa mbele za Mungu.
Baadhi ya wananchi wamesema kukamilika kwa nyumba hiyo kutaokoa familia ya mama huyo aliyekuwa anaishi mazingira hatarishi.
Taasisi ya Tulia Trust hutumia sehemu ya faida kwenye mikopo na usajiri wa michezo ya riadha kuelekeza fedha kwenye jamii.
Mjane huyo ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba iliyoezekwa maturubai yeye na watoto wake sita huku wakipitia changamoto za ya namna ya kuendesha maisha kila siku ya kujikwamua kiuchumi.
Recent Posts
- WANAFUNZI WAMTAJA DKT. TU…August 21, 2024Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]
- WALIOHITIMU ELIMU YA KIDA…August 21, 2024Wanafunzi watano waliokuwa wakisoma nchini Nigeria kwa ufadhiri wa Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wa Spika wa Bunge Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wamewasili leo Ijumaa Agost 16 mwaka huu.[…]
- 1,000 KUSHIRIKI MASHINDAN…August 21, 2024Mashindano hayo yanajulikana kama Tulia Cooking Festival yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi Agosti 2024 na yakishirikisha washiriki 1,000[…]
- WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO…May 22, 2024Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 11, 2024 ameshiriki katika tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathoni 2024[…]
- DKT. TULIA ATOA MSAADA KW…April 22, 2024Dkt.Tulia Ackson amekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa waathirika ambao nyumba zao zilifunikwa na maporomoko ya tope katika Mlimani Kawetele Kata ya Itezi jijini hapa na kusababisha kukosa makazi ya kuishi.[…]