
Muktasari:
- Amesema viongozi waliopo sasa, akiwamo Rais Samia Suluhu Hassan, wana matarajio na dhamira ya kuendelea kuhudumia wananchi, hivyo kuimba wimbo huo kwa sasa kungeweza kuonekana kama ishara ya kutotamani kuendelea na majukumu yao.
Mwanga. Wakati Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akieleza namna alivyoshindwa kuimba wimbo wa “Moyo wangu una furaha ya kwenda mbinguni” katika ibada ya mazishi ya hayati Cleopa Msuya, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, alitumia jukwaa hilo kumkumbuka tukio la mwaka 1990, Msuya alipowasaidia yeye na waziri wake usafiri wa kurudi ofisini, baada ya baraza la mawaziri kuvunjwa wakajikuta hawana usafiri.
Ibada hiyo ya mazishi ilifanyika katika Usharika wa Usangi Kivindu, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakuu wa kitaifa.
Dk Tulia alieleza kuwa hakuweza kuimba wimbo huo kwa sababu ujumbe wake ulihusu utayari wa kwenda mbinguni, jambo ambalo alilihusianisha moja kwa moja na hali ya kisiasa, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
“Niliamua kukaa kimya na kusikiliza kwa makini. Nikasema, nashukuru askofu alituruhusu tusio tayari tusiimbe. Sisi tunaotazamia uchaguzi 2025 hatujaimba, si kwa sababu hatutaki kwenda mbinguni, bali tunaomba kwenda baadaye,” alisema Dk Tulia kwa ucheshi uliopokelewa kwa vicheko na tafakari.
Dk Tulia amesema aliathiriwa sana na ujumbe wa wimbo huo ambao ulizungumzia utayari wa kwenda mbinguni. Wimbo huo namba 157, fungu la tatu, kutoka katika kitabu cha ‘Tumwabudu Mungu wetu uliombwa kuimbwa na Mkuu wa
Kanisa hilo, Askofu Dk Alex Malasusa.
Hata hivyo, Dk Tulia amesema hakushiriki kuimba wimbo huo na alimshukuru Askofu Malasusa kwa kuelewa na kuruhusu wale ambao hawakuwa tayari, kutouimba.
“Kuna neno unasikia na unajua linakuhusu. Kila mmoja amechukua kile kinachomgusa, lakini mimi nilikaa kimya, nikasikiliza kwa makini sana ule wimbo unaosema ‘mbinguni tunao utayari’. Nikaona siwezi kuimba, kwa sababu sina utayari wa kwenda sasa,” alisema Dk Tulia.
“Nashukuru kwa kuturuhusu tusio tayari tusiimbe… Sasa hivi tuna mtazamo na matarajio, tuna Rais wetu Samia Suluhu Hassan ambaye tunamtarajia, na sisi wengine wenye matarajio pia, hatukuimba.”
Recent Posts
NYOTA YA PILTON MUSA YAZI…
July 18, 2025Tulia Trust tunatoa pongezi nyingi sana kwa Aliyekuwa Mshindi wa Kwanza kwenye Mashindano ya Kusaka Vipaji yaliyo anzishwa na Rais wa[…]WANANCHI UYOLE WAMCHUKULI…
July 18, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]DKT.TULIA ATANGAZA KUGOMB…
July 18, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]DK BITEKO: MARATHONI NI F…
July 18, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]MBEYA TULIA MARATHON YAAN…
July 18, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]