DK TULIA AONGOZA WANANCHI MBEYA KUPIMA NA KUTIBIWA MACHO BURE

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk. Tulia Ackson, leo ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya katika zoezi la upimaji macho na utoaji wa matibabu bure.

Zoezi hilo ambalo linatolewa kwa siku tatu mfululizo, limeanza rasmi katika Shule ya Msingi Kagera, iliyopo Kata ya Ilomba, na linatolewa kupitia ushirikiano kati ya Tulia Trust na The Bilal Muslim Mission of Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Dk. Tulia amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo muhimu, akibainisha kuwa afya bora ni msingi wa maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.

“Taasisi ya Tulia Trust itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoa huduma mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi. Afya ya macho ni eneo ambalo wengi hulipuuza, lakini lina athari kubwa kwa maisha na ustawi wa kila siku,” amesema Dk. Tulia.

Huduma zinazotolewa katika zoezi hilo ni pamoja na:

  • Upimaji wa macho
  • Ushauri wa kiafya
  • Utoaji wa miwani
  • Matibabu ya macho kwa wagonjwa watakaobainika na matatizo mbalimbali

Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo ya kuwafikia moja kwa moja katika maeneo yao, wakisisitiza kuwa huduma hiyo imeleta unafuu mkubwa kwa familia nyingi ambazo haziwezi kumudu gharama za upimaji wa macho.

Soma Zaidi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

DONATE

Give us a call or fill in the form below and we'll contact you. We endeavor to answer all inquiries within 24 hours on business days. DONATE BY BANK: Account Name: TULIA TRUST Account Number: 0150226766000 Bank Name: CRDB




    vulkan vegas, vulkan casino, vulkan vegas casino, vulkan vegas login, vulkan vegas deutschland, vulkan vegas bonus code, vulkan vegas promo code, vulkan vegas österreich, vulkan vegas erfahrung, vulkan vegas bonus code 50 freispiele, 1win, 1 win, 1win az, 1win giriş, 1win aviator, 1 win az, 1win azerbaycan, 1win yukle, pin up, pinup, pin up casino, pin-up, pinup az, pin-up casino giriş, pin-up casino, pin-up kazino, pin up azerbaycan, pin up az, mostbet, mostbet uz, mostbet skachat, mostbet apk, mostbet uz kirish, mostbet online, mostbet casino, mostbet o'ynash, mostbet uz online, most bet, mostbet, mostbet az, mostbet giriş, mostbet yukle, mostbet indir, mostbet aviator, mostbet casino, mostbet azerbaycan, mostbet yükle, mostbet qeydiyyat