
Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
WANAFUNZI 3000, kutoka Kata 36, na mitaa 181,jijini Mbeya wanaoishi katika mazingira magumu, wamepatiwa msaada wa vifaa vya shule na taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt . Tulia Ackson (IPU)ili viweze kuwasaidia kuendelea na masomo.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na madaftari, sare za shule,huku ikiwa ni awamu ya pili taasisi hiyo kutoa vifaa hivyo kwa wanafunzi hao, ambapo mwaka 2024 zaidi ya wanafunzi 3000 walipatiwa vifaa kama hivyo.
Mratibu wa taasisi ya Tulia Trust anayeshughulika na masuala ya elimu,Adili Kalinjila,amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikijitahidi kuboresha elimu na maisha ya wananchi wenye uhitaji.
Kalinjila amesema kuwa taasisi hiyo imeanzisha miradi ya kijamii ya kuwainua kiuchumi wananchi,kama vile tamasha la ngoma za jadi, kutoa bima za afya kwa wazee, familia zenye uhitaji pamoja na mashindano ya Tulia Marathon pamoja na mashindano ya kuibua vipaji mtaani.
Pia amesema kwa upande wa elimu, taasisi imekuwa ikitoa sare za shule,kulipa ada na kusaidia matibabu kwa wanafunzi wenye changamoto za kiuchumi.Ambapo mwaka 2024,ilitekeleza zoezi la kugawa sare,madaftari, kwa wanafunzi 3000 kutoka kata 36 za Jiji la Mbeya na mitaa 181, hivyo kufanya jumla ya wanafunzi 6000 kunufaika na msaada huo kwa mwaka 2024 na 2025.
“Zoezi hili ni sehemu ya juhudi ya kuunga mkono sera ya elimu bure,kuhakikisha wanafunzi wanapata vifaa vya msingi vya masomo ili waweze kufanya vizuri.Tulia Trust pia imewezesha wanafunzi zaidi 20, kupata elimu nje ya nchi wakiwemo wanafunzi wanne wanaosoma nchini Nigeria ambao walianza kidato cha kwanza na sasa wamejiunga na elimu ya vyuo vikuu,”amesema Kalinjila.
Amesema lengo ugawaji wa vifaa hivyo ni kutoa msaada kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu, kuhakikisha wanafunzi wa Jiji la Mbeya wanapata elimu bora,kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha sekta ya elimu nchini.
Mmoja wa mwanafunzi aliyepatiwa msaada kutoka shule ya Msingi Iganzo , Elizabeth Mwanakatwe amesema kuwa kitendo alichofanya Dkt.Tulia kimewafuta machozi kwani awali hawakua na sare wala madaftari.
“Namshukuru Dkt.Tulia kwani nilikuwa na daftari moja tu,hali iliyonifanya nisome kwa shida na hata sare za shule zilikua zimechanika hivyo vifaa hivi nitavitunza vizuri na nitasoma kwa bidii,”amesema Elizabeth.
Amani Mwakasege ni Mwalimu wa shule ya Msingi Igoma iliyopo Kata ya Isanga jijini Mbeya, amesema zoezi hilo linasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye familia zisizojiweza na hawana sare shule na daftari,hivyo anaamini kwa sasa wataendelea vyema na masomo na ufaulubwao utaongezeka.
Recent Posts
NYOTA YA PILTON MUSA YAZI…
July 18, 2025Tulia Trust tunatoa pongezi nyingi sana kwa Aliyekuwa Mshindi wa Kwanza kwenye Mashindano ya Kusaka Vipaji yaliyo anzishwa na Rais wa[…]WANANCHI UYOLE WAMCHUKULI…
July 18, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]DKT.TULIA ATANGAZA KUGOMB…
July 18, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]TULIA ASHINDWA KUIMBA WIM…
July 18, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]DK BITEKO: MARATHONI NI F…
July 18, 2025Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]