Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
WANAFUNZI wanaoishi katika mazingira hatarishi Jijini Mbeya wamepatiwa msaada wa madaftari na Taasisi ya Tulia Trust ikiwa ni mwendelezo wa kusaidia jamii kwa kata 36 zilizopo Jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Machi 12,2024 mara baada kukabidhiwa Daftari kwa shule ya msingi Hasanga,Uyole pamoja na Kilimo iliyopo kata ya Uyole Jijini Mbeya,Ofisa Elimu kata ya Uyole ,Mwl.Lucas Komba amesema kwamba msaada uliotolewa na Taasisi ya Tulia Trust utawapa bidii ya kusoma wanafunzi kwani awali walikuwa na mahudhurio hafifu darasani kutokana na kukosa vifaa vya kujifunzia.
“Awali watoto hawa walikuwa na mahudhurio hafifu lakini hivi sasa baada ya kupatiwa vifaa vya kujifunzia ikiwemo Daftari na sare za shule hivi sasa mahudhurio yao yamekuwa mazuri darasani na hata utoro kupungua tunashukuru uongozi wa shule hii ya Hasanga kutoa taarifa za watoto hawa na kuona umuhimu wa kusaidiwa na taasisi ya Tulia Trust “amesema Ofisa Elimu kata hiyo.
Kwa upande wake Ofisa habari na mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust,Joshua Mwakanolo amesema kuwa msaada uliotolewa kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ni ahadi aliyoitoa Spika wa bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson wakati alipokabidhi sare za shule kwa wanafunzi 3000 mwezi January mwaka huu ambapo ilitakiwa wanafunzi hao wapatiwe daftari lakini kutokana na kuchelewa kufika kwa daftari hizo Dkt.Tulia alitoa agizo kwa wanafunzi wote wanaoishi katika mazingira hatarishi wapatiwe mara baada ya kufika vifaa hivyo vya kujifunzia kwa kata 36.
Akielezea zaidi Ofisa habari huyo amesema kuwa katika zoezi hilo jumla ya daftari 600000 zitatolewa kwa kata 36 za Jiji la Mbeya na kuwa zoezi hilo.litakuwa endelevu kwa mkoa wa Mbeya na adhima ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson nimekuona lengo lake linatimia la kusaidia wahitaji.
Hata hivyo Mwakanolo amesema kuwa katika kata ambazo wamekuwa wakipita wamekuwa wakikutana na changamoto ya watu wenye ulemavu huwapatia viti mwendo na Magongo yote ni kuhakikisha kuwa wanawaondolea adhima wategemezi wao kwa kuwabeba mgongoni na kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Aidha Mwakanolo amesema vitimwendo vitatolewa kwa kata 36 za Jiji la Mbeya na kuwa kulingana na uhitaji watarajia kutoa viti mwendo zaidi ya 36 kulingana na uhitaji na kuwa wahitaji ni wengi hawawezi kumaliza wote kwa wakati mmoja.
Aidha Mwakanolo ametaja shule walizofikia mpaka Sasa kuwa ni Mafanikio shule ya msingi ,Mwasote Shule ya msingi, Tambulika Reli Shule ya msingi,Uyole,Hasanga,Kilimo na kwamba lengo ni kufikia kata 36 zote za Jiji la Mbeya.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya msingi Hasanga ,Mwl.Alphonce Mkuchika amesema kuwa shule ya Hasanga ina jumla ya wanafunzi 1,150 na wanafunzi waliopatiwa msaada ni 37 ambao ni kuanzia darasa la kwanza mpaka Darasa la saba nakushukuru kwa msaada huo na kusema watoto hao baadhi yao walikuwa wanashindwa kuandika darasani kutokana na kukosa vifaa vya kujifunzia.
Recent Posts
- WANAFUNZI WAMTAJA DKT. TU…August 21, 2024Watoto watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini...[…]
- WALIOHITIMU ELIMU YA KIDA…August 21, 2024Wanafunzi watano waliokuwa wakisoma nchini Nigeria kwa ufadhiri wa Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wa Spika wa Bunge Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wamewasili leo Ijumaa Agost 16 mwaka huu.[…]
- 1,000 KUSHIRIKI MASHINDAN…August 21, 2024Mashindano hayo yanajulikana kama Tulia Cooking Festival yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi Agosti 2024 na yakishirikisha washiriki 1,000[…]
- WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO…May 22, 2024Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 11, 2024 ameshiriki katika tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathoni 2024[…]
- DKT. TULIA ATOA MSAADA KW…April 22, 2024Dkt.Tulia Ackson amekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa waathirika ambao nyumba zao zilifunikwa na maporomoko ya tope katika Mlimani Kawetele Kata ya Itezi jijini hapa na kusababisha kukosa makazi ya kuishi.[…]