WALIOHITIMU ELIMU YA KIDATO CHA SITA KWA UFADHIRI WA DKT. TULIA NIGERIA WAWASILI NCHINI
Wanafunzi watano waliokuwa wakisoma nchini Nigeria kwa ufadhiri wa Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wa Spika wa Bunge Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wamewasili leo Ijumaa Agost 16 mwaka huu.
Mapokezi hayo yamefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Songwe huku ndugu jamaa na viongozi mbalimbali walishiriki wakiongozwa na Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust Jackline Boaz.
Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo Jackline amesema vijana hao watano akiwepo wa kiume mmoja walikuwa wakiishi katika mazingira magumu na kwamba walipata ufadhiri kuanzia kidato cha kwanza mpaka sita katika moja ya shule nchini Nigeria.
“Wameishi huko kipindi cha miaka sita sasa wamerejea katika likizo fupi baada ya kuhitumu wakisubiri matokeo watarejea tena nchini humo kwa ajili ya kuendelea na elimu ya juu kwa ufadhiri wa Spika Dkt. Tulia” amesema.
Amesema kati ya wanafunzi hao watano wapo waliotoka Mkoa wa Ruvuma huku na kuweka bayana lengo Mkurugenzi wa Taasisi hiyo kuona watoto wenye mazingira magumu wanapata fursa ya kupata elimu bora.
Akizungumza huku akibubujikwa na machozi mara baada ya kugusa ardhi ya Tanzania mmoja wa wanafunzi hao Ayuob Richard (17) amesema Dkt. Tulia amemuinua kutoka chini kupanda juu kufuatia kutoka katika familia duni.
“Mimi tangu nizaliwe nimelelewa na mama nilielezwa baba yangu mzazi alifariki nimeishi maisha duni mpaka Taasisi ya Tulia Trust kupitia Mkurugenzi wake Dkt. Tulia kuniokota na kunipeleka nchini Nigeria ambako nimesoma elimu ya kidato cha kwanza mpaka sita” amesema.
Naye Beauty Jafary amemfanisha Dkt. Tulia na mshumaa uliowashwa ukimulika na kuisha kwani ameweza kuwawezesha kutimiza ndoto zao kwa kuwatoa katika mazingira magumu na kuwapia fursa ya elimu nje ya nchi.
“Niwaombe watanzania Dkt. Tulia ni mshumaa tumlinde na kumnza kwa kumuonyesha upendo, ushirikiano ili aweze kutimiza ndoto yake kwa watanzania na kulifikisha taifa mbali.
https://mbeyapresstv.blogspot.com/2024/08/waliohitimu-elimu-ya-kidato-cha-sita.html
Recent Posts
- Vegas Hero Casino: Zijn d…March 11, 2026Vegas Hero Casino, een dynamische speler in de online gokindustrie, heeft de aandacht getrokken van […]
- True Luck Casino offre-t-…March 7, 2026En tant qu’analyste en ligne spécialisé dans les casinos depuis plusieurs années, j’ai examiné avec […]
- Der Froggybet Kosmos: Ein…March 6, 2026Als SEO-Kopiräfter mit zehn Jahren Erfahrung im iGaming-Bereich habe ich viele Online-Casinos […]
- Lizaro Casino: een diepga…March 6, 2026Het lizaro online casino heeft zichzelf gepositioneerd als een aantrekkelijke optie voor online […]
- De gebruikersinterface va…March 6, 2026Million Casino is een interessante nieuwkomer in de online gokwereld, die zich richt op zowel […]