General Archives - Tulia Trust

WANANCHI UYOLE WAMCHUKULIA FOMU DKT. TULIA ACKSON KUGOMBEA UBUNGE
Wananchi wa Jimbo la Uyole Mkoani Mbeya wamemchukulia fomu ya kuwania Ubunge Dkt. Tulia Ackson katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2025 hapa nchini.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Uyole Adil Mwansepele amesema kilichowasukuma kumchukulia fomu Dkt. Tulia ni mapenzi yake kwa wananchi wa Jimbo hilo jipya la Uyole.

Soma Zaidi

The post WANANCHI UYOLE WAMCHUKULIA FOMU DKT. TULIA ACKSON KUGOMBEA UBUNGE appeared first on Tulia Trust.

DKT.TULIA ATANGAZA KUGOMBEA JIMBO JIPYA LA UYOLE
Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini,Dkt.Tulia Ackson,ametangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo jipya la Uyole mkoani Mbeya katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Dkt.Tulia amesema hayo leo 23 Mei,2025 alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu Maalum wa Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo amesema kuwa ameamua kufanya uamuzi huo ili kuwahudumia wananchi wa Uyole kutokana na kasi ndogo ya maendeleo iliyopo katika eneo hilo.

“Maendeleo ya Uyole yanasonga kwa taratibu sana,nimeona ni vyema nijitoe kwa moyo wote kuhakikisha wananchi wa Uyole wanapata huduma stahiki na maendeleo ya haraka.Nitoe wito kwenu, watu wengi watakuja kwenu, chagueni kiongozi, chagueni mtumishi, itasaidia sana kuendelea kuyakimbiza maendeleo ya jamii,”amesema Dkt.Tulia.

Awali amezishukuru Kata zote thelathini na sita kwa ushirikiano mkubwa waliompatia wakati akitekeleza majukumu yake na kusema maendeleo yanapoletwa katika jamii kuna watu wananufaika na wengine wanapata maumivu.

Aidha  Dkt.Tulia amesema kugawanywa kwa Jimbo ni kusogeza maendeleo kwa wananchi na maombi yalikuwa mengi nchini lakini mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa majimbo nane yaliyogawanywa.

Dkt.Tulia amesema katika kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele atahakikisha majimbo yote mawili yanapaa kimaendeleo na kusema bado ni mzazi wa watoto wote wawili.

Aidha  Dkt.Tulia amesema kuwa Kwa mgawanyiko huo wa Jimbo asiwepo mtu wa kujiona ni zaidi ya mwenzie na kutoa wito kwa wananchi wa Mbeya Mjini kuchagua Viongozi bora wenye hofu ya Mungu watakaochagiza maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya Mjini ,Afrey Nsomba amesema kuwa  Dkt.Tulia amekuwa kiongozi wa mfano , wanawake,vijana na kusema kila siku amekuwa ni daraja,na habagui na kujali makundi yote.

“Leo hii kazi nyingi ulizofanya wewe kama mbunge wetu  na ndo maana hapa kila mmoja hapa anavutia upande wake  lakini kitendawili hiki utakitegua mwenyewe,mh Mbunge sisi wana mbeya  tunakupenda Sana na Mimi niseme kama mwrnyewekiti kokote utakokwenda lazima upite kwa kishindo kikubwa lazima heshima yako iendelee kusimama,kwani umefanya Mbeya yetu kuwa na mabadiliko makubwa”amesema Mwenyekiti huyo.

Akizungumza katika mkutano huo Maalum, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge amesema kuwa  Dkt Tulia amekuwa mtu wa kujali watu na kujitoa hivyo ni jambo ambalo linahitaji moyo wa kipekee Sana na kwamba wana Mbeya wanatakiwa kumpa ushirikiano popote atakapokuwa anaenda.

“Kama chama tunakuhakikishia tutakupa ushirikiano mkubwa kwasababu kazi zako zinajieleza na tutahakikisha unarudi tena kwa kishindo kikubwa,”amesema.

Soma Zaidi

The post DKT.TULIA ATANGAZA KUGOMBEA JIMBO JIPYA LA UYOLE appeared first on Tulia Trust.

TULIA ASHINDWA KUIMBA WIMBO WA MBINGU…
Muktasari:

Amesema viongozi waliopo sasa, akiwamo Rais Samia Suluhu Hassan, wana matarajio na dhamira ya kuendelea kuhudumia wananchi, hivyo kuimba wimbo huo kwa sasa kungeweza kuonekana kama ishara ya kutotamani kuendelea na majukumu yao.

Mwanga. Wakati Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akieleza namna alivyoshindwa kuimba wimbo wa “Moyo wangu una furaha ya kwenda mbinguni” katika ibada ya mazishi ya hayati Cleopa Msuya, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, alitumia jukwaa hilo kumkumbuka tukio la mwaka 1990, Msuya alipowasaidia yeye na waziri wake usafiri wa kurudi ofisini, baada ya baraza la mawaziri kuvunjwa wakajikuta hawana usafiri.

Ibada hiyo ya mazishi ilifanyika katika Usharika wa Usangi Kivindu, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakuu wa kitaifa.

Dk Tulia alieleza kuwa hakuweza kuimba wimbo huo kwa sababu ujumbe wake ulihusu utayari wa kwenda mbinguni, jambo ambalo alilihusianisha moja kwa moja na hali ya kisiasa, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

“Niliamua kukaa kimya na kusikiliza kwa makini. Nikasema, nashukuru askofu alituruhusu tusio tayari tusiimbe. Sisi tunaotazamia uchaguzi 2025 hatujaimba, si kwa sababu hatutaki kwenda mbinguni, bali tunaomba kwenda baadaye,” alisema Dk Tulia kwa ucheshi uliopokelewa kwa vicheko na tafakari.

Dk Tulia amesema aliathiriwa sana na ujumbe wa wimbo huo ambao ulizungumzia utayari wa kwenda mbinguni. Wimbo huo namba 157, fungu la tatu, kutoka katika kitabu cha ‘Tumwabudu Mungu wetu uliombwa kuimbwa na Mkuu wa

Kanisa hilo, Askofu Dk Alex Malasusa.

Hata hivyo, Dk Tulia amesema hakushiriki kuimba wimbo huo na alimshukuru Askofu Malasusa kwa kuelewa na kuruhusu wale ambao hawakuwa tayari, kutouimba.

“Kuna neno unasikia na unajua linakuhusu. Kila mmoja amechukua kile kinachomgusa, lakini mimi nilikaa kimya, nikasikiliza kwa makini sana ule wimbo unaosema ‘mbinguni tunao utayari’. Nikaona siwezi kuimba, kwa sababu sina utayari wa kwenda sasa,” alisema Dk Tulia.

“Nashukuru kwa kuturuhusu tusio tayari tusiimbe… Sasa hivi tuna mtazamo na matarajio, tuna Rais wetu Samia Suluhu Hassan ambaye tunamtarajia, na sisi wengine wenye matarajio pia, hatukuimba.”

Soma Zaidi

The post TULIA ASHINDWA KUIMBA WIMBO WA MBINGU… appeared first on Tulia Trust.

DK BITEKO: MARATHONI NI FURSA KIUCHUMI KWA WAFANYABIASHARA
Muktasari:

Dk Biteko amesema uwepo wa mbio Betika Mbeya Tulia Marathon ni fursa kubwa kwa wafanya bishara, huku akihamasisha umoja na ushirikiano kupitia mashindano hayo.

Mbeya. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Dk Dotto Biteko amesema uwepo wa mashindano ya mbio za Betika Mbeya Tulia Marathon 2025 unachangia kukuza fursa za kiuchumi kwa wafanyabiashara Mkoa wa Mbeya.

Dk Biteko, ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Mei 10, 2025 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mashindano hayo yaliyoanza jana Mei 9, 2025.

Mbali na kufungua mashindano ya mbio hizo, Biteko ameshiriki mbio za kilometa tano akiongozwa na mwenyeji wake, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa mjini, Dk. Tulia Ackson sambamba na viongozi wa chama na serikali.

Amesema uwepo wa mbio hizo ni fursa kubwa kwa wafanya bishara, huku akihamasisha umoja na ushirikiano kupitia mashindano hayo.

“Kuna watu waliibeza, lakini leo ulizeni wafanya bishara wa Mbeya, fursa wanazopata kupitia mashindano ya Tulia Marathoni? Niwatake kuwa wamoja, lakini pia tunaona kuna mwitikio mkubwa wa ushiriki,” amesema.

Wakati huohuo, Dk Biteko, amempongeza Spika Tulia kwa kuandaa mashindano hayo kila mwaka sambamba na kumpatia msanii wa vichekesho, Bosi kimaro kitita cha Sh5 milioni.

“Hongera sana msanii wetu Kimaro kwa mchango wako wa sadaka kwa Wanambeya kuunga mkono mashindano ya mbio za Tulia Marathon kila mwaka,” amesema Dk Biteko.

Katika hatua nyingine, Biteko amesema wanamuombea Dk Tulia kuendelea na kazi hiyo kwa kuendelea kuongoza jimbo la Mbeya.

“Mlishafanya huko nyuma na sisi wabunge tulivyofika bungeni kwa Mbunge wenu tulimfanya kuwa Spika. Lakini alipokwenda duniani Mheshimiwa Rais alisema nileteeni mwanangu wa Mbeya,” amesema Biteko.

Kauli ya Dk Tulia

Kwa upande wake Spika wa Dk. Tulia amesema hizo ni mbio za kipekee nchini na ndio maana zimefanyika kwa siku mbili ambapo leo Mei 10, 2020 wameanzia kilometa 42.

“Kwanza niwashukuru wadau kwa kuungana nasi katika nia njema ya kuboresha miundombinu ya elimu na afya lakini tuishukuru serikali kwa kuboresha sekta ya afya nchini,” amesema.

Dk Tulia amesema katika kuunga mkono jitihada za serikali kwa mwaka huu, wametoa bima za afya kwa wananchi 9,000, na kuwezesha mahitaji kwa watoto kutoka kaya maskini zikiwepo sare za shule na madaftari.

“Nimeanza kuwashukuru wananchi. Walijiandikisha kushiriki mbio hizi kwani ni sehemu ya mchango wa kusaidia watoto mazingira magumu kupata vifaa vya shule kama sare na madaftari,” amesema.

Katika hatua nyingine amesema wanagusa kaya za wazee wasiojiweza kwa kuwajengea makazi bora na mahitaji mengine kama chakula na mavazi.

Dk Tulia amesema kupitia mashindano hayo wamejitokeza wadhamini mbalimbali ikiwepo kampuni ya Betika na Wasaf na Taasisi mbalimbali za kifedha.

Mashindano hayo yameshirikisha mbio za uwanjani za mita 1,500-800-400-200-100 na mita 50 kwa watoto kwa mbio za uwanjani, huku kwa mbio za barabarani ilianzia mita 42.

Naibu Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema msimu huu mashindano yamekuwa na mwamko mkubwa wa ushiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini.

“Binafsi nimekimbia kilometa tano, lakini pia nimewezesha vijana zaidi ya 27 kushiriki mashindano hayo,” amesema Mahundi.

Soma Zaidi

The post DK BITEKO: MARATHONI NI FURSA KIUCHUMI KWA WAFANYABIASHARA appeared first on Tulia Trust.

MBEYA TULIA MARATHON YAANZA KUTIMUA VUMBI
Mashindano ya Riadha ya Betika Mbeya Tulia Marathon 2025 yameanza leo Kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya Mjini ikiwa ni Msimu wa Tisa (9) Mashindano hayo yanafanyika.

Pichani ni baadhi ya Washiriki wa Mashindano hayo ambayo leo yanafanyika kwa mbio za ndani ya uwanja (Mbio Fupi) ambazo ni Mita100, 200, 400, 800, 1500 na Long Jump (Karuka Chini).

Kesho Mashindano haya yataendelea kwa mbio ndefu ambazo ni kilomita 42, 21, 10 na 5.

Soma Zaidi

The post MBEYA TULIA MARATHON YAANZA KUTIMUA VUMBI appeared first on Tulia Trust.

AFUKUZWA MSIBANI KWA KUTELEKEZA MKE NA WATOTO SITA KWA MIAKA 14
Na Manka Damian , JamhuriMedia, Mbeya

KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida wananchi wa kata ya Itezi mtaa wa Gombe Kusini Mkoani Mbeya wamelazimika kumfukuza msibani mwanaume mmoja aitwaye ,Seleman Lukama baada ya kumtelekeza kwa miaka 14,mke wake Anna Anosyesye na watoto wake sita.

Inaelezwa kuwa baada ya kupata taarifa za kifo cha mke wake April 26,2025 mwanaume huyo alijitokeza na kufika nyumbani kwake hapo hivyo na wananchi na uongozi wa mtaa Gombe kuamuru . mwanaume huyo aondoke mara moja kijijini hapo kutokana na kitendo alichofanya cha kutelekeza familia yake kipindi cha miaka 14.

Akizungumza na wananchi msibani hapo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Itezi Gervas Mwaseba alisema katika mchakato wa wawahitaji katika katika kata hiyo ilipendekeza marehemu Anna Anosyesye ajengewe nyumba ya kuishi kutokana na mazingira magumu aliyokuwa akiishi na watoto wake .

“Itatupa mkwalizo mkubwa kama wamemdanyanya kuwa mama huyo alikuwa na mume kwa Imani ile ile huyu marehemu hakuwa na mume hivyo tuwaite wathaminishaji wa nyumba na kuandikwa jina mojawapo la mtoto ambaye ndiye atakuwa mrithi wa nyumba na kulea wadogo zake na huyu mwanaume atafute nyumba ya kuishi nyingine,anatushangaza huyu mwanaume mwezetu ukiacha familia wewe ni mwanaume chotara kwa kweli umetudharirisha wanaume wenzio”alisema mwenyekiti huyo.

Hata hivyo Mwaseba alisema kuwa wanaamini kuwa watoto hao ni yatima wanaendelea kuhudumiwa na chama ,na kusema kuwa watasimamia nyumba inayojengwa chini ya Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na mkurugenzi wake ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson mpaka nyumba kukamilika na hati ya nyumba iandikwe watoto.

Janet Kabuje ni Barozi shina namba tisa kata ya Itezi mtaa wa Gombe kusini amesema kuwa mwanaume huyo alimtelekeza mke wake na watoto sita kwa miaka 14, na kwa kilichofanywa na mwanaume huyo sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye tabia za kutekeleza familia zao .

” Mimi mama Claudia nimechota nae maji Kwenye matololi stendi ya Usangu kwa shida kabla hajaanza kuumwa ambapo maji hayo alitumia kufyatua tofari za kujengea nyumba yake ,huyu baba akiwa hayupo na aliondoka na mwanamke wa hapa hapa mtaani kwetu na huko alikokuwa akiishi alikuwa na maisha mazuri tu huko ,lakini ulichofanya kwa familia yako kwa miaka 14 ,ni kitendo cha aibu Sanaa na ni kweli nilikuona pale hospitali lakini kwa ulichofanya hichi ni kitendo cha aibu leo sheria ichukue mkondo wake ili funzo kwa Wanaume wengine wenye tabia kama hizi “amesema Kabuje.

Mwenyekiti serikali ya mtaa wa Gombe Kusini, Amesema ameanza kuumwa hakuwahi kufahamu kama ana mume na kusema kuwa kabla ya kuanza kuumwa marehemu alienda kwa Mwenyekiti kueleza kukimbiwa na mume na kumuacha na watoto sita .

Aidha amesema baada ya kuhojiwa msibani hapo Mume wa marehemu aliomba msamaha mbele ya waombelezaji msibani hapo na kusema alikuwa anakuja na kuondoka na kusema hana la kuongea zaidi ya kuomba msamaha.

Kitendo alichofanya Mwezetu huyu mwanaume ametudharisha Sana kitendo cha kutekeleza mke na watoto ni cha aibu Sanaa hivyo huyu mwanaume aliona ndoa aliyofuata ndo bora zaidi kuliko familia yake ya mke na watoto sita.

Taasisi ya Tulia Trust ilimwibua Marehemu Anna Anosyesye ilifika nyumbani kwa Anna wakati wa kukimbiza mbio za bendera za upendo katika kata ya Itezi mtaa wa Gombe kusini.

Soma Zaidi

The post AFUKUZWA MSIBANI KWA KUTELEKEZA MKE NA WATOTO SITA KWA MIAKA 14 appeared first on Tulia Trust.

DK TULIA AONGOZA WANANCHI MBEYA KUPIMA NA KUTIBIWA MACHO BURE
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk. Tulia Ackson, leo ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya katika zoezi la upimaji macho na utoaji wa matibabu bure.

Zoezi hilo ambalo linatolewa kwa siku tatu mfululizo, limeanza rasmi katika Shule ya Msingi Kagera, iliyopo Kata ya Ilomba, na linatolewa kupitia ushirikiano kati ya Tulia Trust na The Bilal Muslim Mission of Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Dk. Tulia amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo muhimu, akibainisha kuwa afya bora ni msingi wa maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.

“Taasisi ya Tulia Trust itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoa huduma mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi. Afya ya macho ni eneo ambalo wengi hulipuuza, lakini lina athari kubwa kwa maisha na ustawi wa kila siku,” amesema Dk. Tulia.

Huduma zinazotolewa katika zoezi hilo ni pamoja na:

Upimaji wa macho

Ushauri wa kiafya

Utoaji wa miwani

Matibabu ya macho kwa wagonjwa watakaobainika na matatizo mbalimbali

Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo ya kuwafikia moja kwa moja katika maeneo yao, wakisisitiza kuwa huduma hiyo imeleta unafuu mkubwa kwa familia nyingi ambazo haziwezi kumudu gharama za upimaji wa macho.

Soma Zaidi

The post DK TULIA AONGOZA WANANCHI MBEYA KUPIMA NA KUTIBIWA MACHO BURE appeared first on Tulia Trust.

TAASISI YA TULIA TRUST YAMFUTA MACHOZI BIBI ANAYEISHI KWA KUOKOTA MAKOPO
Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

Mjane Eva Chungu (70) Mkazi wa Mtaa wa Mwanyanje kata ya Igawilo ambaye anaishi  kwa kuokota makopo na mabaki ya mikaa sokoni amefutwa machozi na Taasisi ya Tulia Trust baada ya kuanza hatua ya kumjengea ya nyumba ya kuishi.

Taasisi hiyo inajenga nyumba tatu katika kata tofauti ikiwewo ya Mjane Eva  kutokana na makazi yake ya awali kuwa hatarishi kwa maisha yake.

Aprili 5,2025 wakati Taasisi ya Trust ilipofika nyumbani kwa Chungu kwa ajili kuanza ujenzi wa nyumba yake ameeleza kuwa alikuwa anabeba mabaki sokoni na kuokota makopo na kuuza ili apate fedha za kujikwamua kiuchumi kwa ajili ya kununua mahitaji.

Chungu amesema mbali na changamoto mbalimbali alizopitia aliamua kufyatua tofari na kujenga nyumba ambayo imebomolewa na kujengwa nyingine kufuatia mazingira yake kutokuwa rafiki.

Joshua Mwakanolo ni Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust amesema kuwa ujenzi wa nyumba hizo tatu wahitaji watatu wa mitaa ya Gombe kusini kata itezi ,mtaa wa utukuyu kata ya Uyole pamoja na mtaa wa Mwanjanje kata ya Igawilo ambazo zinategemewa kukamilika ndani ya mwezi mmoja ili ziweze kukabidhiwa kwa wahitaji hao walioibuliwa wakati wa mbio za bendera ya upendo inayoratibiwa na Taasisi hiyo chini ya Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson.

“Mkurugenzi wetu ametoa maelekezo kuhakikisha nyumba zote tatu za  wahitaji zinakamilika ndani ya  mwezi mmoja ili wahitaji hawa waweze kukabidhiwa mapema iwezekanavyo hivyo tutegemee Dkt.Tulia mwenyewe mwezi Mei,mwaka huu atakuja kukabidhi nyumba hizi ambazo idadi yake itakua imefikia 21 kujengwa ndani ya mkoa wa Mbeya na nje ya mkoa wa Mbeya amesema  Mwakanolo.

Aidha Mwakanolo amesema kuwa mpaka sasa nyumba 18, zimejengwa na kukabidhiwa kwa walengwa na kuwa siku ya hiyo kupitia bendera ya upendo kwa siku kadhaa zilizopita ambayo ilikimbikizwa kata ya Uyole, Igawilo  na Itezi  baada ya kukimbiza bendera hiyo waliweza kutoa vyakula,mavazi, mahitaji ya shule na wanafunzi walioshindwa kuendelea na  masomo ambapo Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini aliagiza  kuhakikisha wanahudumiwa vizuri katika kupata mahitaji yote ya msingi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwanjanje, Joseph Ndambo amesema kuwa  mama huyo  alipatikana  wakati  bendera ya upendo ilipopita mitaa minne ya kata ya Igawilo na baada ya kufanya tahlthimi kamati ya maendeleo ya kata ilimptisha mama huyo ili aweze kujengewa nyumba na kupongeza jitihada kubwa za Mbunge wa Jimbo hilo Dkt.Tulia Ackson katika kuona kundi la wahitaji.

Rhoda chengula amesema kuwa mara ya kwanza kumuona bibi huyo alimuona akiokota makopo kwenye maahimo ya kutupa taka ili aweze kuuza na kumsaidia kununua chakula lakini pia  mazingira ya kuishi peke yake yalisababisha vijana kumwingilia usiku na kumbaka.

Jirani mwingine ,Emmanuel Njowele amesema kama majirani walikuwa wa kwanza kutoka kumwangalia  bibi huyo  kwani amekuwa akiishi maisha duni hivyo kushukuru Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake Dkt Tulia Ackson kwa ujenzi wa nyumba hiyo imekuwa mkombozi kwake.

“Kwakweli tunasema Dkt.Tulia Mungu ambariki kwa msaada huu wa ujenzi wa nyumba tunaomba msichoke na kusaidia wengine wenye uhitaji kama wa huyu bibi,” amesema Njowele.

Soma Zaidi

The post TAASISI YA TULIA TRUST YAMFUTA MACHOZI BIBI ANAYEISHI KWA KUOKOTA MAKOPO appeared first on Tulia Trust.

SHEIKH NJALAMBAHA AONYA FIKRA MBAYA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Muktasari:

Kauli hiyo imetolewa na Shekhe wa Mkoa wa Mbeya , Shekhe Msafiri Njalambaha  leo Jumatano Machi 19, 2025 baada ya kupokea futari kwa wahitaji 200 wa dini ya Kiislamu iliyotolewa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Mbeya. Viongozi wa dini ya Kiislamu Mkoa wa Mbeya wamefanya dua maalumu ya kuliombea Taifa na viongozi wa Serikali akiwepo Rais Samia Suluhu Hassan katika kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.

Mbali na dua hilo wakikemea baadhi ya Watanzania kujiepusha na fikra mbaya za kujihusisha uvunjifu wa amani

na badala yake kuombea utulivu na amani kwa maslai ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha ametoa kauli hiyo leo Jumatano Machi 19, 2025 baada ya kufanya dua maalumu na kupokea futari za wahitaji 200 iliyotolewa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kupitia Taasisi ya Tulia Trust.

Njalambaha amesema huu ni mwaka wa uchaguzi kama viongozi wa dini wanalojukumu kubwa kuungana na waumini

na Watanzania kuombea amani, utulivu na kukemea vitendo “Taifa letu limepata tunu ya viongozi wa ngazi za juu

wanawake akiwepo Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya, Dk Tulia Ackson, hivyo niwaombe Watanzania tuzitunze hizi tunu na tusikubali kuzipoteza,” amesema.

Wakati huo huo,Shekhe Njalambaha amewataka wananchi kutohusisha misaada inayotolewa na Mbunge wa Mbeya

mjini, Dk Tulia Ackson na masuala ya kisiasa kutokana na kuelekea kipindi cha uchaguzi. “Hii siyo mara ya kwanza kiongozi huyo kugusa wahitaji kila mwaka anatoa mahitaji katika kipindi cha mfungo wa Idd El-Fitr, niombe tu waumini na Watanzania kuendelea kumuombea na kuliombea Taifa akiwamo Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema.

Amesema matendo yanayofanywa, Dk Tulia kuigusa jamii ya Kimungu na siyo mara ya kwanza kugusa wahitaji.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza la Masheikhe Mkoa, Sheikh Ibrahim Bombo ameishukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa utaratibu wake wa kugusa walengwa huku akiwataka maimamu wa misikiti iliyoguswa kuhakikisha walengwa wanafikiwa. “Tuna kila sababu ya kushukuru kwa mahitaji ya walengwa 200 katika misikiti mbalimbali katika Jiji la Mbeya, jukumu letu ni kuendelea kufanya dua kumuombea,” amesema.

Mwakilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Athuman Kapuya ameshukuru ushirikiano wa viongozi wa dini na kuomba kuendelea kumuombea Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson.

Amesema wataendeleza ushirikiano unaogusa jamii yenye mahitaji katika mfungo na kuelekea Sikukuu ya Idd.

Mnufaika Stumahi Michuzi amesema wataendelea kufanya dua kumuombe Mbunge wa Mbeya, Dk Tulia, Mungu aendelee kumzidishia kutokana na namna anavyojitoa kugusa jamii yenye uhitaji.

Soma Zaidi

The post SHEIKH NJALAMBAHA AONYA FIKRA MBAYA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU appeared first on Tulia Trust.

WANAFUNZI 3000 WENYE UHITAJI WAPATIWA VIFAA VYA SHULE
Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

WANAFUNZI 3000, kutoka Kata 36, na mitaa 181,jijini Mbeya wanaoishi katika mazingira magumu, wamepatiwa msaada wa vifaa vya shule na taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt . Tulia Ackson (IPU)ili viweze kuwasaidia kuendelea na masomo.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na madaftari, sare za shule,huku ikiwa ni awamu ya pili taasisi hiyo kutoa vifaa hivyo kwa wanafunzi hao, ambapo mwaka 2024 zaidi ya wanafunzi 3000 walipatiwa vifaa kama hivyo.

Mratibu wa taasisi ya Tulia Trust anayeshughulika na masuala ya elimu,Adili Kalinjila,amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikijitahidi kuboresha elimu na maisha ya wananchi wenye uhitaji.

Kalinjila amesema kuwa taasisi hiyo imeanzisha miradi ya kijamii ya kuwainua kiuchumi wananchi,kama vile tamasha la ngoma za jadi, kutoa bima za afya kwa wazee, familia zenye uhitaji pamoja na mashindano ya Tulia Marathon pamoja na mashindano ya kuibua vipaji mtaani.

Pia amesema kwa upande wa elimu, taasisi imekuwa ikitoa sare za shule,kulipa ada na kusaidia matibabu kwa wanafunzi wenye changamoto za kiuchumi.Ambapo mwaka 2024,ilitekeleza zoezi la kugawa sare,madaftari, kwa wanafunzi 3000 kutoka kata 36 za Jiji la Mbeya na mitaa 181, hivyo kufanya jumla ya wanafunzi 6000 kunufaika na msaada huo kwa mwaka 2024 na 2025.

“Zoezi hili ni sehemu ya juhudi ya kuunga mkono sera ya elimu bure,kuhakikisha wanafunzi wanapata vifaa vya msingi vya masomo ili waweze kufanya vizuri.Tulia Trust pia imewezesha wanafunzi zaidi 20, kupata elimu nje ya nchi wakiwemo wanafunzi wanne wanaosoma nchini Nigeria ambao walianza kidato cha kwanza na sasa wamejiunga na elimu ya vyuo vikuu,”amesema Kalinjila.

Amesema lengo ugawaji wa vifaa hivyo ni kutoa msaada kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu, kuhakikisha wanafunzi wa Jiji la Mbeya wanapata elimu bora,kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha sekta ya elimu nchini.

Mmoja wa mwanafunzi aliyepatiwa msaada kutoka shule ya Msingi Iganzo , Elizabeth Mwanakatwe amesema kuwa kitendo alichofanya Dkt.Tulia kimewafuta machozi kwani awali hawakua na sare wala madaftari.

“Namshukuru Dkt.Tulia kwani nilikuwa na daftari moja tu,hali iliyonifanya nisome kwa shida na hata sare za shule zilikua zimechanika hivyo vifaa hivi nitavitunza vizuri na nitasoma kwa bidii,”amesema Elizabeth.

Amani Mwakasege ni Mwalimu wa shule ya Msingi Igoma iliyopo Kata ya Isanga jijini Mbeya, amesema zoezi hilo linasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye familia zisizojiweza na hawana sare shule na daftari,hivyo anaamini kwa sasa wataendelea vyema na masomo na ufaulubwao utaongezeka.

Soma Zaidi

The post WANAFUNZI 3000 WENYE UHITAJI WAPATIWA VIFAA VYA SHULE appeared first on Tulia Trust.